
WAZIRI MKUU
WA ZIMBABWE, MORGAN TSVANGIRAI, AMEMLAANI WAZIRI MMOJA WA SERIKALI, AMBAYE
ALITANGAZA KUWA BENKI ZA KIGENI NI SHARTI KUACHIA ASILIMIA KUBWA YA HISA ZAKE
KWA RAIA WA NCHI HIYO KATIKA KIPINDI CHA MWAKA MMOJA UJAO.
BWANA
TSVANGIRAI AMESEMA SERIKALI YA NCHI HIYO HAIJAJADILI AU KUIDHINISHA TANGAZO
HILO.
TVANGIRAI
AMESHUTUMU WAZIRI WA MASUALA YA KITAIFA, SAVIOUR KASUKUWERE, KWA KUSAMBAZA
HABARI ZINAZOASHIRIA KUWA SERIKALI YA NCHI HIYO INANUIA KUNYAKUA UMILIKI WA
KAMPUNI NA TAASISI NCHINI HUMO.
WAANDISHI WA
HABARI WANASEMA SERA HIYO, IMEGAWANYA SERIKALI YA MSETO YA NCHI HIYO,
INAYOSHIRIKISHWA CHAMA CHA BWANA TSVANGIRAI NA CHAMA CHA RAIS ROBERT MUGABE CHA
ZANU PF.
ILITANGAZWA
MAPEMA JUMANNE KUWA BENKI LAZIMA KUZINGATIA SHERIA YA MWAKA 2007 AMBAYO
INASHURUTISHA ASILIMI 51 HISA ZA BENKI ZOTE KUWA MIKONONI MWA RAIA WA NCHI
HIYO.
BENKI KUU NA
WIZARA YA FEDHA ZIMESEMA KUWA HATUA KAMA HII ITAHUJUMU UCHUMI WA ZIMBABWE.
No comments:
Post a Comment