Monday, June 11, 2012

YONDANI AZUA KIZAAZAAAAAAAA


RAIS WA SHIRIKISHO LA SOKA (TFF) LEODGAR TENGA AMEAGIZA KUFANYIKA KWA UCHUNGUZI WA NAMNA AMBAVYO BEKI CALVIN YONDANI WA KLABU YA SIMBA ALITOROKA KWENYE KAMBI YA TAIFA STARS NA KWENDA KUSAINI MKATABA WA KUICHEZEA YANGA.
 AFISA HABARI WA SIMBA EZEKIEL KAMWAGA ALISEMA WAMEPOKEA BARUA YA TENGA AKIWATAARIFU VIONGOZI WA KLABU HIYO KUWA AMEAGIZA KUFANYIKA UCHUNGUZI HUO.
KWA MUJIBU WA KAMWAGA, TENGA ANATAKA KUFAHAMU NAMNA MCHEZAJI HUYO ALIVYOONDOKA KWENYE KAMBI YA TIMU YA TAIFA NA KWENDA KUSAINI MKATABA NA YANGA USIKU WA KUAMKIA ALHAMISI WIKI HII.
UONGOZI WA SIMBA, AMESEMA KAMWAGA, UMEPOKEA KWA FURAHA TAARIFA HIYO YA RAIS WA TFF.
“BAADA YA BARUA YA TENGA AMBAYO AMEELEZA KUFANYA UCHUNGUZI JUU YA YONDANI IKIWA NI PAMOJA NA USAJILI WAKE, SISI TUMEAMUA SASA KUKAA KIMYA JUU YA SUALA HILI,” ALISEMA KAMWAGA.
ALISEMA UONGOZI WA KLABU HIYO KWA SASA UMELIACHA SUALA LA YONDANI MIKONONI MWA TFF HUKU AKISISITIZA KUWA MCHEZAJI HUYO NI MALI YA KLABU HIYO.
KAMWAGA ALISEMA KATIKA BARUA AMBAYO TENGA AMEIANDIKIA SIMBA, AMEAHIDI UCHUNGUZI UTAFANYIKA KATIKA MAENEO MAKUU MAWILI.
ENEO LA KWANZA NI IWAPO NI KWELI YONDANI ALIONDOKA KAMBINI USIKU NA KWENDA KUSAINI MKATABA YANGA, NA IWAPO ALIONDOKA KWA RUHUSA MAALUMU AU ALITOROKA. PIA TFF ITACHUNGUZA USAJILI WA MCHEZAJI HUYO KUJUA NI MALI YA TIMU GANI.
ENDAPO YONDANI ATAGUNDULIKA ALITOROKA ADHABU ITAWAFIKIA WOTE WALIOHUSIKA KATIKA SAKATA HILO, TENGA ALIAHIDI KWA MUJIBU WA KAMWAGA.
YONDANI AMEKUA GUMZO BAADA YA KUDAIWA KUSAINI MKATABA KWENYE KLABU MBUILI ZA SIMBA NA YANGA HUKU PIA AKITUHUMIWA KUTOROKA KWENYE KAMBI YA TIMU YA TAIFA

No comments:

Post a Comment