Wednesday, June 13, 2012

RAIS MWINGINE UARABUNI AHUKUMIWA


SHIRIKA LA HABARI LA TUNISIA LINASEMA RAIS WA ZAMANI WA NCHI HIYO ZINE EL ABIDINE BEN ALI AMEHUKUMIWA MIAKA ISHIRINI JELA KWA KUHUSISHWA NA MAUAJI YA VIJANA WANNE MWEZI JANUARI MWAKA JANA.
BW BEN ALI HAKUWEPO MAHAKAMANI.
ALIKIMBILIA SAUDI ARABIA MWAKA JANA BAADA YA VUGUVUGU LA MAGEUZI YA KIRAIA AMBAYO BAADAYE YAMEONEKANA KUWA NI MAPINDUZI YA KIARABU.
HUKUMU YA KIFUNGO CHA MIAKA 20 JELA ILIPITISHWA NA MAHAKAMA YA KIJESHI MJINI TUNIS. KIONGOZI HUYO WA ZAMANI ZINE EL ABIDINE BEN ALI TAYARI ALIKUA AMEISHA HUKUMIWA KIFUNGO CHA MIAKA 35 JELA IKIWA BADO ANAKABILIWA NA MASHTAKA MENGINE MENGI.
YEYE NA MKE WAKE WANAKABILIWA NA WARANTI YA KIMATAIFA KUKAMATWA, LAKINI SAUDI ARABIA HAIJAJIBU OMBI LA WAKUU WA TUNISIA LA KUTAKA WAREJESHWE NYUMBANI.
HUKUMU HII INATOLEWA WAKATI SERIKALI MPYA YA TUNISIA INAJITAHIDI KUZIMA MAANDAMANO YANAYOENDELEA NCHINI KOTE.
HAPO JANA JUMANNE KIJANA MMOJA RAIA WA TUNISIA FEHMI AL-AOUINI, ALIUAWA KWA KUPIGWA RISASI KUFUATIA GHASIA ZA SIKU TATU.
MOJA KWA MOJA SERIKALI IKATANGAZA SHERIA YA KUTOTOKA NJE KATIKA MAENEO NANE KUTOKANA NA MACHAFUKO YALIYOSABABISHWA NA MAONESHO YA PICHA AMBAYO CHINI YA IMANI YA KIISLAMU NI HARAMU NA HILO LIKASABABISHA VITUO KADHAA VYA POLISI KUCHOMWA MOTO.
SERIKALI ILIYALAUMU MAKUNDI YANAYOJULIKANA KAMA WA SALAFI KWA KUCHOCHEA GHASIA. AMBAZO WANDISHI WAMEZIELEZEA KAMA GHASIA MBAYA KUWAHI KUTOKEA NCHINI TUNISIA TANGU MAPINDUZI YALIYOMNGATUA MADARAKANI BEN ALI MWAKA JANA.
HATA HIVYO WA SALAFI WAMEKANUSHA KUHUSIKA.
MAHAKAMA YA KIJESHI ILIYOSIKILIZA KESI YAKE ILIMPATA PIA KUA NA HATIA YA UFUJAJI WA FEDHA ZA UMMA, RUSHWA NA KUMILIKI DAWA HARAMU PAMOJA NA SILAHA BILA KIBALI.
KATIKA KESI FUPI YA HIVI KARIBUNI, WANA USALAMA KADHAA WALIHUKUMIWA VIFUNGO VYA MDA MFUPI KWA KUHUSIKA KATIKA MAUWAJI YA VIJANA WANNE HUKO OUARDANINE.

No comments:

Post a Comment