Sunday, June 10, 2012

RAIS MWAI KIBAKI ATANGAZA SIKU 3 ZA MAOMBOLEZO KUFUATIA VIFO VYA MAWAZIRI
WAZIRI wa Usalama  nchini  Kenya Profesa George Saitoti na Naibu wake Orwa Ojode pamoja na  maofisa wengine watano wamefariki dunia katika ajali ya helikopta ya polisi iliyotokea  jana nchini humo iliyoanguka msituni.
Mawaziri hao ambao waliambatana na  maofisa wengine wa juu katika Wizara ya usalama walikuwa wakielekea katika eneo la Sotik kwa ajili ya  mkutano wa usalama.
Saitoti alikuwa miongoni mwa wanasiasa mashuhuri nchini Kenya waliokuwa wakipania kugombea kiti cha urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Ajali hiyo ya kusikitisha ilitokea  majira ya asubuhi katika eneo la Kibiku, karibu na mji wa Ngong  kilometa ishirini kutoka mji mkuu wa Nairobi.
Taarifa zilisema kwamba Helikopter hiyo ya polisi ambayo ilikuwa imebeba abiria saba wote walipoteza maisha kiasi ambacho hawakuweza kutambulika.
Walioshuhudia ajali hiyo walisema waliona helikopta hiyo ikizunguka angani kabla ya kuanguka katika msitu wa Ngong. 
Baada ya kutokea ajali hiyo Polisi walilizingira eneo la ajali huku kamishna wa polisi Mathew Iteere ambaye na yeye pia alikuwapo katika eneo hilo alisema kwamba atatoa taarifa kamili kuhusiana na ajali hiyo kwa waandishi wa habari.
Ni miaka minne tu tangu kutokea kwa ajali nyingine ya Helkopta ambapo awali ilikuwa mwezo Juni 10 2008,ambapo mawaziri wawili wa nchi hiyo walipoteza maisha.
Mawaziri ambao walipoteza maisha katika ajali hiyo ni pamoja na  , Kipkalya Kones na Lorna Laboso ambao walifariki mwezi Juni 10, 2008 kwa ajali ya helkopta.No comments:

Post a Comment