Friday, June 15, 2012

MAONI JUU YA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2012-2013

MBOWE


MWENYEKITI WA CHADEMA, FREEMAN MBOWE ALISEMA: “HAKUNA MKATABA WA MAKUSUDI WA KUPUNGUZA MATUMIZI YA SERIKALI, AHADI YAKE YA KUPUNGUZA MATUMIZI KWA KUPUNGUZA POSHO ZISIZO NA TIJA NA MATUMIZI MENGINE HAIKUTEKELEZWA.”
MBOWE AMBAYE PIA NI KIONGOZI WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI, ALISEMA AMESHANGAZWA NA KUTOKUWAPO KWA NYONGEZA YA MISHAHARA KWA WATUMISHI WA UMMA NA BADALA YAKE FEDHA NYINGI KURUNDIKWA KATIKA MATUMIZI YA KAWAIDA YA SERIKALI.

LIPUMBA
“UTAWALA UNAGHARIMIWA KWA SH10 TRILIONI HALI UWEZO WA KUKUSANYA MAPATO YA NDANI NI SH8 TRILIONI, HII INAMAANISHA KWAMBA SERIKALI YETU PIA INATUMIA FEDHA ZA WAHISANI KUGHARIMIA MATUMIZI YA KAWAIDA

MBATIA


“HUWEZI KUCHUKUA FEDHA ZOTE UKAURUNDIKIA UTAWALA HALAFU UKAWAACHA WANANCHI BILA KITU, HICHO NDICHO TULICHOKIONA LEO, SH10 TRILIONI NI KWA AJILI YA MISHAHARA NA WATUMISHI NA MATUMIZI YA KAWAIDA, MAENDELEO AMBAKO NDIKO WANANCHI WALIKO KUMEACHWA TENA KUTEGEMEA FEDHA ZA WAFADHILI,”


LISSU
 “MWAKA JANA WAMEKUJA NA BAJETI KAMA HII YA KUTEGEMEA FEDHA ZA WAFADHILI, ZAIDI YA ASILIMIA 40 YA FEDHA ZILIZOTENGWA HAZIKUPATIKANA NA LEO WANAKUJA NA BAJETI YA AINA ILEILE,” 

OLE TELELE
BAJETI HII NI PIGO KUBWA KWA WAFUGAJI KWANI WAMESHINDWA KUTENGEWA FEDHA KWA AJILI YA KUBORESHA UFUGAJI HASA WALE AMBAO WANAHAMAHAMA.

GRATIAN MUKOBA

“KWA KWELI NI KIASI KIDOGO SANA, TENA IMETUVUNJA NGUVU, KWA SABABU TULITEGEMEA WAFANYAKAZI TUTAPEWA KIPAUMBELE KWENYE BAJETI, LAKINI KILICHOTOKEA NI TOFAUTI KABISA,”

DEUS KIBAMBA
BAJETI YA MWAKA HUU IMEENDELEA KUWA YENYE MANUFAA KWA VIONGOZI WA SERIKALI NA KUWAUMIZA WANANCHI WA HALI YA CHINI.
ALISEMA HAIWEZEKANI BAJETI YA MWAKA 2006/7 IKAWA ZAIDI YA SH4 TRILIONI HALAFU YA MWAKA 2012/13 IKAFIKA SH15.2 TRILIONI NA BADO IKAWA HAINA MANUFAA KWA WANANCHI.








No comments:

Post a Comment