Thursday, June 14, 2012

KIM WA STARS ALONGO


TAIFA STARS IKAKABILIANA NA MSUMBIJI(MAMBAS) KATIKA PAMBANO LA MARUDIANO KUSAKA NAFASI YA KUFUZU FAINALI ZA MATAIFA YA AFRIKA LITAKALOPIWA JUNI 17 KWENYE UWANJA WA ZAMPETO JIJI LA MAPUTO.
KIM ALISEMA JANA KUWA HAFURAHISHWI NA UTAMADUNI WA BAADHI YA WACHEZAJI KUKAA NA MPIRA MUDA MREFU AKISEMA AINA HIYO YA UCHEZAJI INATOA FURSA KWA WAPINZANI KUJIPANGA.

"KWA UJUMLA NAWEZA KUSEMA TUPO TAYARI KWA MAPAMBANO NA KUISHINDA MSUMBUJI NA KUSONGA MBELE, TUMEFANYA MAZOEZI MEPESI LAKINI HASA NILIKUWA NAKAZANIA UFUNGAJI.
"NIMEWAMBIA WACHEZAJI WANGU HAKUNA SABABU YA KUKAA NA MPIRA MUDA MREFU, SAMATA(MBWANA) AMEKUA TABIA YA 'ANAOANAO' MPIRA, MATOKEO YAKE ANACHOKA,"ALISEMA KIM.
"NATAKA MCHEZAJI ANAPOPATA MPIRA AANGALIE KISHA ATOE PASI NA KUFUNGUA KAMA ANAVYOFANYA BOBAN(HARUNA). YEYE NI MFANO MZURI AKIPATA MPIRA ANAANGALIE KISHA ANAPIGA PASI SEHEMU HUSIKA,".
AIDHA, MDENMARK HUYO ALISEMA KUWA, KUREJEA KWA BAADHI YA WACHEZAJI WAKE WALIOKUWA MAJERUHI AKIWAMO NURDIN BAKAR, SHAABAN NDITI NA BEKI AGGREY MORRIS KUMEONGEZA NGUVU KATIKA KIKOSI CHAKE.

No comments:

Post a Comment