Saturday, June 16, 2012

HATMA YA AL-SHABAAB SHAKANI


 
JENERALIL ABDULLAHI ALI AGEY, KAMANDA WA KIKOSI CHA PILI CHA JESHI LA SOMALIA, ALISEMA WANACHAMA WA AL-SHABAAB WANAOGOPA HATIMA ISIYOJULIKANA KWA SABABU WANAHISI MABADILIKO MAKUBWA YA KUIREJESHA SERIKALI NA KUIMARISHA JESHI NA TAASISI ZA USALAMA KUTOKANA NA MPANGO MKUU.
KIJESHI, KIKUNDI WASHIRIKA WA AL-QAEDA KINAKABILIWA NA MZOZO MKUBWA BAADA YA KUIPOTEZA AFGOYE NA VITONGOJI VYAKE, NA INAONEKANA KUWA KIKO KATIKA UKINGO WA KUIPOTEZA BANDARI YA KISMAYO, AMBAYO NI KITOVU CHA KIFEDHA.
AGEY ALISEMA JESHI LA SOMALIA, KWA MSAADA KUTOKA VIKOSI VYA AFRIKA, VITAENDESHA MASHAMBULIZI YA HALI YA JUU KATIKA WIKI ZIJAZO KATIKA JARIBIO LA KUWAZUIA VIONGOZI WA AL-SHABAAB.
AL-QAEDA WANAKABILIWA NA VIPINGAMIZI VINGI. KARIBUNI TULIMUDU KUPATA MAFANIKIO KWA SABABU TULIINGIA KATIKA NGOME ZAO IMARA NA HAKUWEZA KUTUZUIA,” ALIIAMBIA SABAHI. "TULIELEWA WAZI JUU YA MGAWANYIKO WAO MKUBWA NDANI YA KIKUNDI CHENYE SIASA KALI NA KARIBUNI TUTAWEZA KUITEKA MIJI ILIYOKO KATIKA UDHIBITI WAO."
AGEY ALISEMA, WANACHAMA WA AL-SHABAAB WANAKIMBILIA MILIMA YA GOLIS NA KUSINI MWA YEMEN.
ALISEMA AL-SHABAAB IKO KATIKA HALI MBAYA NA KIKUNDI KINACHOKUFA, KAMA AMBAVYO BAADHI YA WANACHAMA WAKE WAMEELEZEA KUTORIDHIKA KWAO NA UTENDAJI WA KIKUNDI.
OPERESHENI ZA PAMOJA BAINA YA JESHI LA SOMALIA NA AMISOM KARIBUNI WAMEONGEZA MASHAMBULIZI SOMALIA KOTE, NA KUPELEKEA KWA VIFO NA MAJERUHI KWA WAPIGANAJI WENGI KUTOKA KWA KIKUNDI CHENYE MAFUNGAMANO NA AL-QAEDA.
JENERALI ABDI MAHDI ABDISALAM, KAMANDA WA OPERESHENI KATIKA ENEO LA JUBA YA CHINI, ALISEMA KUWA AL-SHABAAB WANAWASIWASI KUHUSU USHINDI WA VIKOSI VYA SERIKALI KATIKA MAJIMBO YA SHABELLE YA CHINI NA JUBA YA CHINI.

No comments:

Post a Comment