Sunday, December 4, 2011

Warusi wamaliza kupiga kura


Watu wa Urusi wamepiga kura kuchagua bunge, yaani Duma, la miaka mitano ijayo.


Katika maeneo mengine ya Arctic wapigaji kura walijitokeza katika kipimo cha baridi cha nyuzi 26 chini ya sufuri.

Mwandishi wa BBC mjini Moscow anasema uchaguzi huu unachukuliwa kama kura ya maoni juu ya Waziri Mkuu, Vladimir Putin, ambaye atagombea urais tena mwezi wa March.

Upigaji kura ulipokuwa unaendelea wasimamizi wa kujitegemea walilalamika kuwa wanaingiliwa kati na wakuu.

Vituo kadha vya redio na makundi ya upinzani, yalisema kuwa tovuti zao ziliingiliwa na kufungwa.

Na televisheni ya taifa inasema kuwa chama cha Vladimir Putin, Waziri Mkuu, kimepata kura kidogo kushinda uchaguzi uliopita.

Inasema kuwa kura za maoni hadi sasa zinaonesha kuwa chama cha United Russia, kilipata asili mia 48.5 ya kura.

No comments:

Post a Comment