Friday, December 2, 2011

MKUU WA MASHTAKA WA JACOB ZUMA AKATALIWA

Mahakama moja ya Afrika Kusini imeharamisha hatua ya Rais Jacob Zuma ya kumteua Menzi Simelane kuwa mkuu wa mashtaka.
Mahakama hiyo imesema kuwa kuna mambo fulani kumhusu Simelanea ambayo yanatilia dosari sifa yake, kwani kuna wakati alitoa ushahidi wa uongo.
Chama cha Upinzani cha Democratic Alliance (DA) kilikuwa kimewasilisha kesi ikidai kuwa Bwana Simelane ni kibaraka wa Bwana Zuma.
Chama hicho kiliambia mahakama kuwa Simelane angeliwalinda watu fulani mashuhuri kutokana na kushitakiwa
Lakini Rais Zuma amekuwa akikanusha madai hayo huku akishikilia kuwa Bwana Simelane alikuwa ana sifa na uwezo wa kishikilia wadhifa huo wa mkuu wa mashitaka wa Afrika Kusini. Zuma pia alisema kuwa ilikuwa haki yake kama rais kuamua ni nani anastahili kuwa mkuu wa mashitaka na hiyo sio kazi ya mahakama.
Jaji wa Mahakama ya juu zaidi ya Rufaa Mahomed Navsa amesema kuwa kuteuliwa kwa Simelane kuwa Mkurugenzi wa Mashitaka ilikuwa kinyume cha katiba ya nchi.
Kiongozi wa chama cha upinazi cha DA Helen Zille ametaja uamuzi wa mahakama kama ushindi kwa demokrasia.
Amesema katika siku za hivi karibuni rais Zuma amekuwa akifanya uteuzi uliojaa utata ukiwemo uteuzi wa jaji Mkuu.

No comments:

Post a Comment