Ben
Komba/Pwani-Tanzania/14-4-2014
Mvua kubwa zilizonysha kwa
siku tatu mfululizo zimeathiri kwa kiasi kikubwa shughuli mbalimbali za
uzalishaji mali katika mkoa wa Pwani, ambapo barabara kuu ya Morogoro madaraja
mbalimbali yametitia kutokana na mvua hiyo kubwa ambayo imesababisha madhara
makubwa kwa miundombinu.
Mwandishi wa habari hizi ameshuhudia msongamano mkubwa wa malori na magari ya abiria yakiwa yamejipanga kufuatia kukatika kwa kipande cha barabara eneo la Ruvu na kusababisha magari kushindwa kupita eneo hilo na kuzxua foleni kubwa ambayo imeanza kupitisha magari madogo.
Nayo serikali
haikuwa nyuma kupitia kikosi cha ujenzi barabarani imefanya kazi kubwa
kukarabati maeneo ambayo yamekumbwa na uharibifu uliosababishwa na mafuriko
makubwa ya maji ambayo yalifunika kabisa barabara ya Morogoro na kufanya
shughuli za usafirishaji na uchukuzi kusimama kwa takriban masaa 72.
Uharibifu
huo haukubaki barabara kubwa ya Morogoro, bali hata shamba la ushirika la
kilimo cha umwagiliaji Ruvu wilayani Bagamoyo-CHAURU- nalo limeathirika kwa
kiasi kikubwa na mvua hizo, kwa madaraja mawili kukatika na kuwafanya wakulima
kuamua kutumia jitihada zao kukarabati maeneo korofi huku wakiitaka serikali
kutupia macho madhara yaliyosababishwa na mvua hizo.
Makamu
mwenyekiti wa ushirika huo wa kilimo mpunga kwa njia ya umwagiliaji-CHAURU-
BW.MSIRIKAL;I amebainisha kuwa mpaka sasa wameomba makaravati kutoka ofisi ya
mkuu wa mkoa wa Pwani ili waweze kukarabati maeneo korofi na kuepukana na adha
zilizoletwa na mvua hiyo.
Akizungumzia uharibifu wa mazao hususan ya mpunga, BW.MSERIKALI amebainisha kuna uwezekano mkubwa wa kupungua kwa mavuno iwapo mvua hizi zitaendelea, kwani mpaka sasa kuna uharibifu mkubwa wa matuta ya mifereji ambayo inatumika katika shamba hilo.
Ameiomba
serikali kupitia wataalamu wake kuungana na wanachama wake kusaidiana kurudisha
hali ya barabara hiyo inayotumika kuingia na kutoka shamba hilo ambalo ni maarufu
kwa kilimo cha mpunga kwa njia ya umwagiliaji.
No comments:
Post a Comment