Afisaa
mmoja mkuu wa kundi la kigaidi la Alshabaab, amefahamisha BBC kuwa kundi hilo
ndilo limehusika na shambulizi dhidi ya duka la kifahari la Westage mjini
Nairobi Kenya.
Kwa mujibu wa Afisaa
huyo mashambulizi hayo yalikuwa ya kulipiza kisasi kwa Kenya kwa kujihusisha na
vita vya Somalia ambako wanajeshi wake wanakabiliana na kundi hilo.
Wanajeshi wa Kenya
wamekuwa nchini humo tangu mwaka 2011 kama sehemu ya juhudi za muungano wa
Afrika kutaka kurejesha uthabiti nchini Somalia.
Afisaa mkuu wa mambo
ya ndani Kenya amesema idadi ya waliofariki ni kumi na moja lakini shirika la
msalaba mwekundu linasema idadi hiyo imefika watu 30 huku zaidi ya hamsini
wakijeruhiwa.
Taarifa kutoka Ikulu
ya Rais Kenya zinasema kuwa mshukiwa mmoja aliyekamatwa alifariki kutokana na
majeraha yake.
Baadhi ya watu
waliofanikiwa kukimbilia usalama wao
Wanamgambo wa Al
Shabaab kupitia kwa mtandao wao wa Twitter , wanasema kuwa Kenya haikuchukulia
kwa uzito onyo walilotoa kwa taifa hilo kwa hatua ya kuwapeleka wanajeshi wake
nchini humo kupambana dhidi yao.
Kundi hilo limesema
limekuwa likitoa onyo mara kwa mara kwa Kenya kuwa ikiwa haitaondoa vikosi
vyake nchini Somalia, athari zitakuwa mbaya mno.
Kupitia mtandao wao wa
Twitter, Al Shabaab limesema kuwa Kenya ilijidai kutosikia onyo hizo, na
kuendelea kuwaua waisilamu wasio na hatia nchini Somalia.
Taarifa hiyo ya
Twitter ilisema kuwa Shambulio la Westgate ni tone tu katika bahari ya mfano wa
yanayowakumba wasomali nchini Somalia.
Taharuki ilianza hii
leo saa saba mchana wakati watu wanaokisiwa kuwa kumi walipovamia jengo la
kifahari la Westgate la kuwapiga risasi kiholela wakenya waliokuwa wanaendelea
na shughuli zao za kawaida.
Kwa mujibu wa shirika
la msalaba mwekundu , takriban watu 30 walifariki kwa kupigwa risasi au
kutokana na majeraha yao na wengine wengi wenye majeraha ya risasi kukimbizwa
hospitalini kwa matibabu.
No comments:
Post a Comment