Sheikh Ponda Issa Ponda, nimejulishwa kwamba amefariki dunia
kufuatia kushambuliwa kwa risasi na polisi huko Morogoro. Inna Lillah Wainna
illaih raajiun.
Ninalaani kwa nguvu zote matumizi ya nguvu yanayofanywa na
jeshi la Polisi dhidi ya Raia. Hili ni tukio lingine kati ya matukio
yaliyotangulia kuhusu polisi kuua raia hovyo kwa kutumia risasi za moto. Ni
lazima kuendelea kupambana na hali hii. Hata hivyo, ninaomba Watanzania wabakie
watulivu kwani matukio kama haya ni majaribu makubwa kwa Umoja wa nchi yetu.
Mungu ailaze mahala pema peponi roho ya Sheikh Ponda Issa Ponda
No comments:
Post a Comment