ADAM UKOWAPI WEWE?
MWANZO 3: 9 Bwana MUNGU akamwita Adamu,
akamwambia, Uko wapi?
Sote
tunajua yakuwa MUNGU anauwezo wa kutuona popote tulipo iwe juu ya dari,
kichakani, chumbani ma sehemu yoyote ile. Lakin ni vema tuka jiuliza swali hili
ni kwanini MUNGU alimuuliza Adam swali hili MWANZO 3: 9 BWANA MUNGU AKAMWITA
ADAMU, AKAMWAMBIA, UKO WAPI?
Je , ni nini kilitokea?
Ukisoma kitabu cha mwanzo 3 utaona kulikua na mazungumzo ya
nyoka (shetani) na mwanamke ambapo matokeo yake ni wengi tunayajua na
inasadikiwa yametuathiri hadi leo hii. Lakin ukweli ni kuwa katika hali ya
kawaida kumshawishi mwanamke ili afanye jambo lolote ambalo hakulipanga
inahitaji muda mrefu ili aweze kulielewa na kulifanya hivyo katika hali ya
kawaida inawezekana ilimchukua nyoka (shetani) muda mrefu pengine siku kadhaa
akijaribu kumshawishi mwanamke hadi akafanikiwa
lakin katika muda wote huo hatukuambiwa adam alikuwa wapi? Ukisoma
MWANZO 2:18 Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake,
nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye. Kwa maana watakuwa wana saidiana katika
mambo mbalimbali hivyo popote alipo Adam alitakiwa aidha mkewe awepo au ajjue
alipo mumewe, halikadhalika na Adam alitakiwa ajue alipo mkewe muda na saa
yoyote. Je ni kitu gani kilitokea hadi
Adam hakujulikana alipo na mkewe akadanganywa na shetani?
Je
nani alaumiwe?
Je
tumlaumu mwanamke kwa kukubali kukaa kitako na kuongea na shetani (nyoka) kwa
muda wote wa mazungumzo yao bila kumshirikisha mumewe?
Au
Tumlaumu
Adam ambaye yeye alipewa maelekezo na MUNGU na kukabidhiwa mwanamke ili amlinde
na yeye akashika mambo mengine na kuacha KUSIMAMA KATIKA NAFASI YAKE
Kwa
leo tumlaumu Adam kwamaana kama ingekua amesimama vyema katika nafasi yake basi shetani asingelipata nafasi ya kukaa na
kumshawishi mke wa Adam. Lakin pia baada ya nyoka kumrubuni Hawa ilipaswa Adam
kama kiongozi akatae kulila lile tunda kutokusimama katika nafasi yake pia yeye
kama kiongozi alipaswa asijifiche lakin arudi mbele za MUNGU kwaajili ya TOBA
ili kusawazisha mambo yake na MUNGU.
THEME
Sisi
kama binadamu MUNGU ametuita katika nafasi mbalimbali na tofauti tofauti
ilituyatimize malengo mbalimbali ambayo ndio makusudi ya uwepo wetu hapa
duniani lakini sisi tumekua “BUSY” na mambo mengine yanayotupendeza machoni
petu hatakama ni kinyume na kusudi la MUNGU.
HIVYO
KWAKUWA
UWEPO WAKO NI SULUHISHO LA JAMBO FULANI KATIKA MAISHA HAYA SIMAMA KATIKA NAFASI
YAKO ILI ULITATUE JAMBO KATIKA JAMII YAKO.
IKIWA
Ikiwa
hujui kusudi la kuishi kwako ulimwenguni rudi katika sala kwa kuomba ikibidi
kufunga ili KUSUDI LA MUNGU KATIKA MAISHA YAKO LITIMIE.
MUNGU
ANASEMA.
1 WAKORINTHO 2: 8 lakini,
kama ilivyoandikwa, Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia,
(Wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu,) Mambo ambayo Mungu aliwaandalia
wampendao.
9 Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho
huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.
WARAKA WANGU KWA WAPENDWA WOTE (N0 3)
MARKO MANGARA MATHIAS
No comments:
Post a Comment