Msajili wa vyama vya Siasa nchini amewaasa wanachama na
viongozi wa Chama Cha Democrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutumia muda wao
kufanya shughuli za siasa ili kuchangia maendeleo ya nchi badala ya kutumia
uwezo na muda wao kubuni mambo yanayoleta mtafaruku na kuhatarisha amani ya
nchi.
Pia amepinga tamko la chama hicho la kuanzisha mafunzo ya
kujilinda kwa vijana wake nchi nzima.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo
jijini Dar es Salaam na kusainiwa kwa niaba ya Msajili wa vyama vya siasa Sisty
Nyahoza alisema kuwa hajawahi kuruhusu CHADEMA au chama chochote cha siasa
kufanya mafunzo ya ukakamavu au mafunzo ya kutumia nguvu ya aina yoyote kwa
wanachama wake au mtu yeyote yule.
Anaongeza kuwa CHADEMA wanaruhusiwa kuanzisha vikundi vya
kujilinda lakini hawaruhusiwi kuanzisha mafunzo ya kutumia nguvu kwaajili ya
kujilinda kama walivyo tangaza katika mikutano yao ya hadhara kwani ni kinyume
na Demokrasia na Katiba ya Jamuhuri ya Muungano.
Nyahozo ametoa ufafanuzi kuhusu vikundi vya ulinzi na usalama
vilivyopo katika Katiba ya Vyama vya Siasa kwamba vikundi hivyo haviruhusiwi
kufanya mafunzo ya kutumia nguvu ya aina yoyote katika kutekeleza majukumu yao.
Bali wajibu wao ni kutoa taarifa wa vyombo vya Dola pale
wanapo sikia au kuona uhalifu ukitokea na wala sio kupambana na wahalifu au
watu wanaotaka kuwadhuru kama tamko la CHADEMA la tarehe 9 mwezi huu linavyo
sema.
"Hakuna maelezo yoyote katika Katiba ya CHADEMA
yanayoruhusu kutumia nguvu kufanikisha shughuli za kulinda mali na Viongozi wa
Chama.Ni vyema wananchi wote waelewe kuwa Sheria za Nchi zimeweka masharti
maalumu kwa Vyama Vya Siasa kutokana na umuhimu wa vyama hivi katika kudumisha
aman utulivu na umoja wa Kitaifa", alisema Nyahoza.
Alisema kuwa kutokana na Ibara ya20(2)C ya Katiba ya Jamuhuri
ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1997 inasema kuwa "Bila kujali masharti
ya ibara ya (1) na (4),haitakuwa halali kwa chama chochote cha siasa
kuandikishwa ambapo kutokana na katiba au sera yake:-kinakubali au kunapigani
matumizi ya nguvu au mapambano kama njia za kufikia malengo yake ya kisiasa.
Nyahoza alimaliza kwa kuwataka CHADEMA kuacha kutekeleza
mpango walio tangaza wa kuanzisha makambi ya kufanya mafunzo ya kujilinda kwa
vijana wao nchi nzima,kwani kufanya hivyo ni kukiuka sheria za nchi na endapo
watashindwa kutii agizo hilo hatua za Kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
No comments:
Post a Comment