MCHEZAJI WA
KIUNGO CHA KATI WA BOLTON, FABRICE MUAMBA AMETANGAZA KUWA AMESTAAFU KAMA
MCHEZAJI WA KULIPWA WA SOKA.
MUAMBA,
MWENYE UMRI WA MIAKA 24, ALIZIRAI NA KUPATA MSHUTUKO WA MOYO TAREHE KUMI NA
SABA MWEZI MACHI MWAKA HUU WAKATI BOLTON ILIPOKUWA IKICHUANA NA TOTTENHAM
HOTSPURS.
AKIONGEA NA
WAANDISHI WA HABARI MUAMBA, ALISEMA LICHA YA HABARI HIZO KUWA ZA KUHUZUNISHA,
ANAWASHUKURU MASHABIKI WAKE NA WASIMAMIZI WA KLABU HIYO.
''NAMSHUKURU
MUNGU KUWA NIKO HAI HII LEO NA KWA MARA NYINGINE NAWASHUKURU SANA MADAKTARI
WOTE AMBAO HAWAKUFA MOYO WAKATI NILIKUWA NA MATATIZO'' ALISEMA MUAMBA.
No comments:
Post a Comment