Thursday, August 23, 2012

WAHADZABE WATAKA GONGO NA BANGI ILI WAHESABIWE.

ULE MSEMO USEMAO UKISHANGAA YA MUSA UTAYAONA YAFIRAUNI UNAZIDI KUSHIKA KASI, BAADA YA BAADHI YA WAUMINI WA DINI YA KIISLAM KUWA NA MSIMAMO MKALI WA KUTOKUBALI KUHESABIWA MPAKA KIPENGELE CHA DINI KIWEPO, JAMII YA WAHADZABE INAYOISHI PEMBENI YA ZIWA EYASI WAMESEMA HAWATOHESABIWA HADI PALE SERIKALI ITAKAPO TIMIZA SHARTI LAO LA KUTAKA WAPATIWE NYAMA YA NYANI AU NGEDERE ILI WASHIRIKI KATIKA ZOEZI HILO.

DAUDI NTIBENDA AMBAYE NI MKUU WA WILAYA YA KARATU ALITHIBITISHA HAYO NA KUSEMA. "JAMAA WANATAKA NYAMA YA NYANI, GONGO NA BANGI, UNAJUA HAWA WATU WANATAKA KUWE NA JAMBO FULANI KUBWA NDIPO WAKUSANYIKE NA MAKARANI WAWEZE KUPATA IDADI YAO. LAKIN HATA HIVYO TULIWAKATALIA OMBI LAO KWAKUA KWA SASA KULINGANA NA TARATIBU HATURUHUSIWI KUWINDA NYANI, TUMBI NA JAMII YA WANYAMA HAO. LAKIN TULIWAAMBIA TUTAWAPELEKEA NYAMA YA PUNDA MILIA NA TAYARI TUMESHA AGIZA TIMU YA UWINDAJI IKAFANYE ZOEZI HILO".

No comments:

Post a Comment