Thursday, July 12, 2012

MMH MIMI SIJASEMA NIMEI-COPY NA KU-PASTE HAPA


 
DAR ES SALAAM: TAARIFA MBAYA ZINAZOMHUSISHA RAIS JAKAYA KIKWETE NA TOPE LA RUSHWA NA UFISADI ZIMESAMBAZWA KATIKA MITANDAO YA INTANETI TANGU MTANDAO WENYE UTATA MKUBWA WA WIKILEAKS ULIPOCHAPISHA ‘CABLES’ MPYA ZINAZOIHUSU SERIKALI YA TANZANIA.
NILISEME HILI MAPEMA KABISA KWAMBA, WATU TUNAOITAKIA MEMA NCHI HII NA TUNAOIHESHIMU TAASISI TAKATIFU YA URAIS AMBAYO KWA SASA INASHIKILIWA NA RAIS KIKWETE TULIFADHAISHWA NA TAARIFA HIZO ZA WIKILEAKS.
HAUHITAJI KUWA SHABIKI WA RAIS KIKWETE ILI UFADHAISHWE NA TAARIFA AMBAZO ZINAMTUHUMU MOJA KWA MOJA KIONGOZI WAKO MKUU WA TAIFA NA MASUALA YA HOVYO AMBAYO KAMA YATAACHWA KAMA YALIVYO NA HATA KUFIKA HATUA YA KUAMINIKA, YANAWEZA KUENDELEA KUIPOROMOSHA HADHI YA URAIS WA NCHI NAP ENGINE TAIFA ZIMA.
HIVI NANI HAJUI KWAMBA NI AIBU YA TAIFA NA SI YA MTU MMOJA PEKE YAKE, KUWA NA KIONGOZI AMBAYE THAMANI YAKE NI ZAWADI YA SUTI TANO ALIZOPEWA NA MWEKEZAJI MMOJA. HAYA NI MATUSI. HII NI FEDHEHA.
NI KUTOKANA NA UKWELI HUO BASI, NDIYO MAANA SIKUSHANGAZWA HATA KIDOGO NA HATUA YA MAAFISA WANAOSHUGHULIKIA MASUALA YANAYOHUSU MAWASILIANO KATIKA OFISI YA RAIS (IKULU) WAKIONGOZWA NA MKURUGENZI WAO, SALVATORY RWEYEMAMU WALIPOPATA WAKATI MGUMU KUJIBU TUHUMA NZITO ZILIZOELEKEZWA KWA RAIS.
MAOFISA WA IKULU WANGEKUWA NI WATU WA HOVYO KABISA, IWAPO WANGEAMUA KWA MAKUSUDI AU KWA BAHATI MBAYA KUZIPUUZA AU KUJIFANYA HAWAZIJALI, TAARIFA ZA KUMCHAFUA RAIS AMBAZO ZILIANZA KUSAMBAA KWA KASI KUBWA KUPITIA KATIKA KURASA MBALIMBALI ZILIZO KATIKA MITANDAO YA INTANETI NA AMBAZO AGHALAB ZINGEDAKWA AU ZILISHAANZA KUNASWA NA VYOMBO VINGINE VYA HABARI NCHINI.
UTAKUWA NI MTU MPUUZI TU UNAYEWEZA KUYADHARAU AU KUYAPUUZA MANENO AU MAONI YA MWANADIPLOMASIA WA HADHI YA MICHAEL RITZER ALIYEKUWA BALOZI WA MAREKANI HAPA NCHINI ANAYEAMINIKA KUWA CHANZO CHA TAARIFA HIZO AMBAZO KWA MUJIBU WA IKULU ZILIKUWA ZIKILENGA KUMPAKA MATOPE RAIS KIKWETE.
NI JAMBO LA BAHATI MBAYA SANA KWAMBA, IKULU ILIYOJITOKEZA KUMTETEA KAMA SI KUMSAFISHA RAIS KIKWETE DHIDI YA TUHUMA ZA KUPATA KUPOKEA HONGO YA KUSAFIRISHWA KWENDA ULAYA NA KUNUNULIWA ZAWADI YA SUTI TANO WAKATI AKIWA WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, INAFANYA HIVYO WAKATI HUU HADHI YAKE KATIKA JAMII IKIWA NI YENYE KUTIA SHAKA SANA.
SINA SABABU YA KUANZA KUELEZA AU KUFAFANUA HICHO NINACHOKIITA HADHI INAYOTIA SHAKA YA IKULU ZAIDI TU YA KUSEMA KWAMBA, UNAHITAJI KUWA NA AKILI ZA MWENDAWAZIMU KUTAMKA KWA KUJIAMINI LEO HII KWAMBA IKULU YA ZAMA ZA KIKWETE INAZO SIFA ZA KUITWA; ‘MAHALI PATAKATIFU’.
UKILIACHA HILO LA HADHI YA IKULU, UTETEZI NA UFAFANUZI ULIOTOLEWA NA SALVA NA WASAIDIZI WAKE KUHUSU TUHUMA ZINAZOELEKEZWA KWA RAIS NA AMBAZO ZIMESHAANZA KUONEKANA MACHONI MWA BAADHI YA WATU KUWA NI ZA KIPUUZI, KWA MARA NYINGINE UMETHIBITISHA KWA MARA NYINGINE TENA KIWANGO CHA UBINAFSI ULIOVUKA MIPAKA CHA OFISI YA RAIS.
SALVA NA TIMU YAKE, KWA SAUTI ZA KUKARIPIA WAMEZIITA TUHUMA ZINAZOELEKEZWA KWA RAIS KUWA NI UPUUZI USIOPASWA KUAMINIKA NA UZUSHI WENYE LENGO LA KUMPAKA MATOPE RAIS KIKWETE.
UTETEZI ULIOFANYWA NA SALVA KWA KIKWETE JUZI, UNAFANANA NA ULE ULIOPATA KUTOLEWA NA KATIBU MKUU KIONGOZI, PHILEMON LUHANJO KWA NYAKATI MBILI TOFAUTI WAKATI ALIPOJITOKEZA KWA NGUVU KUBWA KUMTETEA RAIS ZAMA JINA LAKE LILIPOHUSISHWA KATIKA SAKATA LA RICHMOND NA DOWANS.
WAKATI SALVA AKIKANUSHA TUHUMA ZINAZOELEKEZWA KWA KIKWETE NA KUSEMA HAZINA UKWELI NA ZIMEJAA UONGO NA VIASHIRIA VINAVYOLENGA KUCHAFUA JINA ZURI NA HESHIMA YA MHESHIMIWA RAIS, ANAONEKANA KUSAHAU AU KUWEKA KANDO FALSAFA YA TUHUMA KUWA KIPIMO TOSHA CHA UWAJIBIKAJI ANAYOIAMINI KIONGOZI ANAYEMTETEA.
SITAKI KUAMINI HATA KIDOGO KWAMBA, IKULU INAMTETEA KIONGOZI AMBAYE KWA KAULI NA MATENDO YAKE NDANI YA VIKAO VYA SERIKALI ANAYOIONGOZA NA HATA KATIKA CHAMA AMBACHO YEYE NI MWENYEKITI WAKE AMETHIBITISHA KWAMBA, NI MTU ANAYEAMINI KWA DHATI KABISA KWAMBA TUHUMA PEKE YAKE ZINATOSHA KUMFANYA KIONGOZI AKAONDOKA MADARAKANI.
HIVI SALVA NA WASAIDIZI WAKE HAWAJUI KWAMBA, DHANA NZIMA YA KUJIVUA GAMBA YA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM) ILIYOASISIWA NA KUABUDIWA NA KIKWETE BINAFSI NA KISHA AKAISIMAMIA KWA MATENDO NDANI YA VIKAO, MZIZI WAKE UKO KATIKA KUZIHESHIMU TUHUMA AMBAZO HATA HAZIJATHIBITISHWA NA MAHAKAMA?
IWEJE LEO SALVA AFIKIE HATUA YA KUITISHA KIKAO CHA WAANDISHI WA HABARI NA KUMTAKA YEYOTE ALIYE NA USHAHIDI WA TUHUMA DHIDI YA RAIS KWAMBA, ALIPATA WAKATI WOWOTE KUPOKEA ZAWADI AU HONGO AKAUWASILISHE USHAHIDI ALIONAO BADALA YA KUMSHAURI MTUHUMIWA MWENYEWE KUPIMA NA KUWAJIBIKA?
HIVI HUYU ANAYETUHUMIWA LEO KUPITIA WIKILEAKS SI KIKWETE HUYO HUYO AMBAYE NDANI YA VIKAO VYA KAMATI KUU NA HALMASHAURI KUU AMEONYESHA UJASIRI WA KUFANYA KILE ALICHOPATA KUFANYA MFALME KAISARI ALIYEMUACHA MKEWE KWA TUHUMA TU ZA UASHERATI HATA BAADA YA UCHUNGUZI KUFANYWA NA KUTHIBITIKA KWAMBA HAKUWA NA HATIA?
HIVI HUYU KIKWETE AMBAYE TUNAAMBIWA ANATUHUMIWA LEO KUPOKEA HONGO AU RUSHWA KUTOKA KWA MMILIKI WA HOTELI YA KEMPINSKI KILIMANJARO HAONI KWAMBA ANAPASWA KUWA MFANO WA KUIGWA KWA KUWAONYESHA NJIA WANASIASA WENZAKE WA NDANI YA CCM AMBAO HATA BAADA YA KUTUHUMIWA BADO WANAENDELEA KUKATAA KUONDOKA NDANI YA CHAMA HICHO?
NI KWA NINI BASI ANASHINDWA KUWA MFANO KWA KUWAONYESHA WANA CCM WENZAKE NAMNA KIONGOZI MWENYE TUHUMA NZITO ANAVYOPASWA KUFANYA.
HIVI TUHUMA ANAZOKABILIANA NAZO KUPITIA WIKILEAKS HAZIFANANI NA ZILE AMBAZO MIEZI MICHACHE TU ILIYOPITA ZILISABABISHA ALIYEKUWA MKURUGENZI WA SHIRIKA LA FEDHA LA KIMATAIFA (IMF) AKAJIUZULU? NI KWA NINI MWASISI WA DHANA YA KUJIVUA GAMBA ANALIKATAA GAMBA AMBALO KWA BAHATI MBAYA LIMEMNASA MWENYEWE?
NI WAZI KWAMBA, JEURI YA AKINA SALVA KUMTETEA KIKWETE IMEJENGWA KATIKA MSINGI MKUBWA MMOJA. WOGA WA WANACHAMA WA CCM AMBAO WAMEUFANYA KUWA UTAMADUNI WA MUDA MREFU WA KUWAHESHIMU VIONGOZI WAO WAKUU HATA KATIKA MAMBO AMBAYO WANAJUA KABISA KWAMBA, VIONGOZI HAO WAMEFANYA MAKOSA YA WAZI.
HIVI NANI HAJUI KWAMBA, HATA KABLA YA TUHUMA HIZI ZA WIKILEAKS AMBAZO MARAFIKI ZA KIKWETE KAMA AKINA ABDULRAHMAN WANAMTETEA, JINA LA KIONGOZI WAO KIPENZI LIMEPATA KUTAJWA PIA, TENA MARA NYINGI TU KATIKA KASHFA NYINGI NYINGINE ZA UFISADI?
JE, WANADHANI TUMESAHAU KUWA KAMA WANAVYOFANYA LEO AKINA SALVA HAO HAO WALIPATA KUFANYA HIVYO HIVYO WAKATI ALIPOTAJWA KATIKA SAKATA LA UFISADI WA IPTL MIAKA YA 1990?
AU WANADHANI SOTE TUMEPOTEZA KUMBUKUMBU NA HATUJUI KWAMBA, HATA KATIKA KASHFA YA EPA KUPITIA KAMPUNI YA KAGODA INAYOAMINIKA KUIBA FEDHA NA KUINGIZA KATIKA KAMPENI ZA URAIS WA CCM WA MWAKA 2005 JINA LA KIONGOZI WANAYEMTETEA LEO HALIWEZI KUACHWA KATIKA MAZINGIRA YA HAKI NA KWELI?
JE, KUNA MTANZANIA ANAYEFUATILIA MASUALA YA KISIASA NA AMBAYE AMEFANYA UTAFITI WAKE WA KINA AMBAYE HAJUI KWAMBA, KWA AKILI ZA KAWAIDA KABISA, HUWEZI UKALITENGANISHA JINA LA KIKWETE (TENA MOJA KWA MOJA) KATIKA SAKATA ZIMA LA RICHMOND NA DOWANS LILILOMLAZIMISHA ALIYEKUWA WAZIRI MKUU NA RAFIKI YAKE MKUBWA KISIASA, EDWARD LOWASSA NA MAWAZIRI WENGINE WAWILI KUJIUZULU?
HIVI WAKATI SALVA NA WASAIDIZI WAKE WANAPOJITOKEZA LEO NA KUMTETEA KWA NGUVU KUBWA, KIKWETE KATIKA SAKATA JIPYA LA WIKILEAKS WANADHANI TUMEYASAHAU MANENO ALIYOPATA KUYASEMA ALIYEKUWA MWENYEKITI WA KAMATI TEULE YA BUNGE ILIYOCHUNGUZA SAKATA HILO LA RICHMOND NA DOWANS, DK. HARRISON MWAKYEMBE?
NITAWAKUMBUSHA. ALISEMA  IWAPO KAMATI TEULE YA BUNGE ALIYOIONGOZA INGEAMUA KUYAWEKA HADHARANI MAMBO YOTE WALIYOBAINI WAKATI WA UCHUNGUZI WAO BASI SERIKALI NZIMA INGEANGUKA!
IKUMBUKWE KWAMBA, MWAKYEMBE ALIYASEMA MANENO HAYA WAKATI TAYARI WAZIRI MKUU AMESHAJIUZULU KWA HIYO NI WAZI KWAMBA, KAULI YAKE HIYO ILIKUA IKIELEKEZWA KWA MTU MMOJA TU; RAIS KIKWETE. NI KWA NINI HAKUANGUKA? KWA NINI HAANGUKI LEO?
IWAPO MWAKYEMBE ALIKUWA ANA MAANA TOFAUTI NA HIYO, AJITOKEZE LEO HII NA KUWAAMBIA WATANZANIA, ALIKUWA AKIMAANISHA NINI WAKATI ALIPOTOA MATAMSHI HAYO AMBAYO KWA SABABU YA KUBEBWA NA UPEPO WA USHABIKI NA UNAZI WA KISIAASA WA MAKUNDI YA NDANI YA CCM KAULI YAKE HAIKUPATA KUPEWA UZITO HATA NA WABUNGE MAHIRI WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI ZAMA ZA BUNGE LA TISA.
WASWAHILI WANA MSEMO WAO MAARUFU; MWOSHA HUOSHWA. LEO NI ZAMU YA KIKWETE AMBAYE HATA BAADA YA JINA LAKE KUTAJWA KWA TUHUMA TU KATIKA IPTL, KISHA EPA (KAGODA), RICHMOND NA SASA WIKILEAKS ANAENDELEA KUSAFISHWA NA KUTETEWA ETI KWA KUWA TU YEYE NI MKUU WA NCHI.
KIKWETE NA WASAIDIZI WAKE WANAPASWA KUJIFUNZA KUTOKA KWA RAIS MSTAAFU, BENJAMIN MKAPA AMBAYE ALILAZIMIKA KUJITOA MHANGA NA KUMTETEA KWA UJASIRI MKUBWA WAZIRI MKUU WAKE, FREDERICK SUMAYE ALIYEKUWA AKIKABILIWA NA TUHUMA ZA KUPIKWA ZA UFISADI.
UTETEZI HUO ALIOUFANYA MKAPA KWA MSAIDIZI WAKE MKUU, ULIVUNJA NGUVU YA GENGE AMBALO SIJAPATA KULIUNGA MKONO HATA MARA MOJA LA MTANDAO AMBALO HAKUNA SHAKA NDILO LILILOKUWA NYUMA YA TUHUMA DHIDI YA SUMAYE NA WANASIASA WENGINE ZAMA ZA SERIKALI YA AWAMU YA TATU.
KIKWETE KWA KAULI NA MATENDO HALITAKI HILO. ANAJIONA YEYE PEKE YAKE. ANAAMINI KATIKA DHANA ILIYOPATA KUMPONZA MZEE CLEOPA MSUYA ISEMAYO; ‘KILA MTU ATABEBA MZIGO WAKE MWENYEWE.’ KATIKA MISINGI YA UONGOZI INAYOAMINI KATIKA UWAJIBIKAJI WA PAMOJA HILI HALIWEZEKANI. KIKWETE NA AKINA SALVA WANAJIDANGANYA.
NI WAZI KWAMBA KIKWETE AMETHIBITISHA PASIPO SHAKA KWAMBA, AMEKUWA NI MTU WA ‘KUSHANGILIA’ KILA MARA WANAPOSHAMBULIWA WANASIASA WENZAKE NDANI NA NJE YA CCM.
AKIWA MKUU WA NCHI, RAIS WA SERIKALI YA JAMHURI YA MUUNGANO, AMIRI JESHI MKUU WA VIKOSI VYA ULINZI NA USALAMA NA MWENYEKITI WA TAIFA WA CCM, KIKWETE AMEKUWA KIMYA NA WAKATI MWINGINE AKIFANYA MASIHARA YA WAZI WAKATI VIONGOZI WENZAKE WANAPOSULUBIWA HATA KATIKA MAKOSA AMBAYO AMA WALIFANYA KWA PAMOJA AU WANAZUSHIWA KWA SABABU TU ZA KISIASA.
TABIA YAKE YA KUWAACHA VIONGOZI WENZAKE WASULUBIWE NA KUWATWISHA MZIGO WA KUJITETEA WAO WENYEWE HATA KATIKA MAMBO AMBAYO SERIKALI INAWAJIBIKA MOJA KWA MOJA, NDIYO ILIYOSABABISHA KWA ZAIDI YA MIAKA SITA SASA SERIKALI IKWAME NA IELEMEWE NA TUHUMA AMBAZO BAADHI YAKE HAZINA MASHIKO.
MATOKEO YA TABIA YAKE YA KUTAKA YEYE PEKE YAKE NDIYE AONEKANE AKIWA SAFI NA SALAMA NDIYO AMBAYO IMEWAFANYA MAADUI NA MARAFIKI ZAKE WAMWITE KILA AINA YA JINA BAYA.
WAKO WALIOMWITA MSALITI, WENGINE WAKAMPACHIKA JINA LA MSANII NA WENGINE KWA SABABU YA KUKATISHWA TAMAA NA AINA YAKE HII YA UONGOZI USIOJALI MAMBO AU UNAOPUUZIA MASUALA YA MSINGI, WAKAMUONA KUWA NI KIONGOZI MSWAHILI. SIFA HIZI HASTAHILI KUWA NAZO KIONGOZI MWENYE DHAMANA KUBWA NA NZITO KAMA ALIVYO YEYE.
YEYE NA TIMU YA WASAIDIZI WAKE IKULU, SERIKALINI NA NDANI YA CHAMA ANACHOKIONGOZA WANAPASWA KUTAMBUA KWAMBA NI JAMBO LISILOWEZEKANA KUWAITA KILA WANAOMTUHUMU YEYE KUWA NI WAZUSHI ISIPOKUWA TU PALE WANAPOTUHUMIWA VIONGOZI WENGINE. HANA SABABU HATA MOJA YA KUSUBIRI KUJIFUNZA KWA VIBOKO.
ORIGINALLY PUBLISHED IN TANZANIA DAIMA NEWSPAPER 07.09.2011

No comments:

Post a Comment