Sunday, July 8, 2012

LIBYA NA UCHAGUZI BAADA YA GADDAFI


Mwanamke akisubiri kupiga kura mjini Tripoli, Jumamosi
ISHARA ZA AWALI ZA MATOKEO YA UCHAGUZI WA MWANZO WA TAIFA KUFANYWA LIBYA KWA KARIBU NUSU KARNE, ZINAONESHA KUWA MUUNGANO WA VYAMA VISIVOKUWA VYA KIDINI, UNAONGOZA KWENYE MAJIMBO MUHIMU, PAMOJA NA TRIPOLI NA BENGHAZI.
 AFISA WA DARAJA YA JUU KATIKA MUUNGANO WA VYAMA, UITWAO NATIONAL FORCES ALLIANCE, ALISEMA RIPOTI ZA AWALI ZINAONESHA KUWA WAO WANAONGOZA KATIKA UCHAGUZI HUO ULIOFANYWA JUMAMOSI, KAULI AMBAYO IMETHIBITISHWA NA KIONGOZI MMOJA WA CHAMA KINACHOWAPINGA, CHA ISLAMIST JUSTICE.
MAAFISA WA UCHAGUZI WANASEMA, MATOKEO RASMI HAYATAJULIKANA KWA SIKU KADHA.
KATI YA VITI 200 VYA BUNGE, VYAMA VYA SIASA VITAPATA VITI 80 TU.
VILIVYOBAKI VITAKUWA VYA WAJUMBE WANAOJITEGEMEA.
<

No comments:

Post a Comment