Saturday, May 26, 2012

UCHAGUZI MISRI




Mohammed Mursi na Ahmed Shafiq

Mgombea wa urais kutoka mrengo wa Muslim Brotherhood Mohammed Mursi anatarajiwa kuchuana na Waziri Mkuu wa zamani Ahmed Shafiq katika raundi ya pili kutokana na matokeo ya kura hadi sasa.

Huku vituo 11,000 kati ya 13,000 zikiwa zimetangaza matokeo yake, Bw Mursi ameongoza kwa asili mia 26 ya kura naye Bw Shafiq amepata asili mia 24. Hamdin Sabbahi mbaye mkosoaji mkubwa wa uliokuwa utawala wa Mubarak anashikilia nafasi ya tatu.
Taarifa zinazohusiana
Afrika

Bw Musri anawakilisha mrengo mashuhuri ambao ulitengwa katika ulingo wa kisiasa kwa miaka mingi chini ya utawala wa Hosni Mubarak.Wagombea wawili wa kwanza wanawakilisha makundi mawili nchini Misri.

Shafiq anatajwa na wakosoaji wa Mubarak kama kibaraka wa utawala ulioondolewa madarakani.

Wadadisi wamesema ameungwa mkono na kundi la watu wanaohofia utawala wa vyama vinavyoegemea sera za kidini na wale ambao wanapinga msukosuko ambao umekuwepo kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Mwandishi wa BBC mjini cairo anasema wagombea walioongoza maandamano ya kumuondoa madarakani Mubarak katika medani ya Tahrir Bw Sabbahi na aliyekuwa Mkuu wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu Amr Mussa waligawanya kura za wafuasi wao.

Raundi ya pili ya uchaguzi wa urais ni mwezi Juni. Asili mia 50 ya wapiga kura wameshiriki uchaguzi wa sasa wa urais nchini Misri.

No comments:

Post a Comment