Wednesday, May 16, 2012

Taylor: Mashahidi walinunuliwa


Rais wa zAmani wa Liberia Charles Taylor
Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor anayetuhumiwa kwa makosa ya kivita amewashambulia waendesha mashtaka kuwa waliwalipa mashahidi wa upande wa mashtaka ili wamkandamize.
Taylor ambaye alikutwa na hatia mwezi uliopita alisema hayo wakati akitoa maelezo kwenye mahakama ya Kimataifa ya makosa ya Jinai ya The Hague.
Hiyo ni nafasi yake ya mwisho ya kujieleza katika mahakama hiyo kabla ya kusomewa hukumu baadae mwezi huu.
Taylor alipatikana na hatia ya kuwasaidia waasi nchin Sierra Leone wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe ambapo pia anaelezwa alisaidia kuendesha mipango ya mauji.
Akitoa maelezo yake Taylor amesema fedha imechukua nafasi katika kesi yake.
"Mashahidi wamelipwa , wamelazimishwa na kwa wakati fulani walitishiwa na waendesha mashtaka kama wasingetoa ushahidi unaonikandamiza", alisema.
Amesema yeye mara zote alikuwa akilaani maauaji popote duniani na aliwahurumia waathirika wa mauaji hayo.
Nje ya mahakama Taylor mara zote amekuwa akipinga makosa yote 11 yanayomkabili huku akisisitiza kuwa hana hatia yoyote.

No comments:

Post a Comment