Thursday, May 17, 2012

MILIPUKO NIGERIA


Ramani ya Nigeria
Takriban watu wawili walioshukiwa kuwa wezi waliojihami, wameuawa baada ya bomu walilokuwa wamemeba kulipuka katika mji wa, Port Harcourt. Taarifa hii ni kwa mujibu wa polisi wa eneo hilo.
Mwandishi wa BBC aliyekuwa kwenye eneo la tukio, anasema kuwa basi walimokuwa wanasafiria, limeharibiwa vibaya sana na mlipuko huo. Watu wengine wawili wako katika hali mahututi hospitalini.
Mkuu wa polisi amesema hakuna sababu ya kuhusisha mlipuko huo na kundi haramau la Boko Haram.
Boko Haram nalo limefanya mashambulizi mengi tu hapo mbeleni kaskazini mwa Nigeria lakini halijalenga maeneo ya mafuta kusini mwa nchi.
Makundi mengine ya wapiganaji yalikuwa yanafanya mashambulizi dhidi ya viwanda vya mafuta mjini Port Harcourt na maeneo yanayozingira mji huo. Lakini wengi sasa wamejiunga na mpango wa serikali ambapo wapiganaji wamekuwa wakisamahewa . Kutoka wakati huo, eneo hilo linasemekana kutulia.

No comments:

Post a Comment