Friday, May 18, 2012

MGOMBEA BINAFSI MBELE KWA MBELE


Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusu mchakato wa Katiba, jijini Dar es Salaam jana. Picha na Rafael Lubava
Fidelis Butahe
HALMASHAURI Kuu ya Taifa (Nec) ya CCM imebariki rasmi kuwapo kwa mjadala wa mgombea binafsi katika mchakato wa kuandikwa Katiba mpya, ikiwa ni siku chache baada ya chama hicho tawala kuwataka wanachama wake kujiandaa kisaikolojia kukabaliana na wagombea hao katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.

Uamuzi huo ni moja ya mambo yaliyoamuliwa katika kikao cha Nec, kilichomalizika juzi mjini Dodoma chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete.

Kwa muda mrefu, kumekuwa na shinikizo kutoka kwa watu wa kada mbalimbali, wakiwamo wanaharakati na wanasheria wanaotaka kuruhusiwa kwa kwa mgombea binafsi jambo ambalo pia liliwahi kupigiwa debe na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1995.

Jana, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu  maazimio ya kikao hicho cha Nec, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya CCM, Nape Nnauye alisema, “ Hatuna tatizo na suala la mgombea binafsi, jambo hili linajadilika, ni mambo ambayo Nec imeona kuwa yanahitaji mjadala mpana zaidi.”

No comments:

Post a Comment