Friday, May 18, 2012

MAMBO YA NGELEJA SIO BONGO PEKEE HATA HUKO JAPAN

Serikali ya Japan imeyataka maeneo ya biashara na kaya nchini humo kupunguza matumizi yao ya umeme kufikia asilimia kumi na tano.
Japan inakabiliwa na upungufu wa umeme baada ya kuzimwa mitambo yake yote ya nyuklia ipatayo hamsini.
Imani ya wananchi kuhusu usalama wa nyuklia imeyumba kutokana na tukio la mtambo wa Fukushima kuyeyuka, hali iliyochochewa na tsunami ya mwaka jana.

No comments:

Post a Comment