Sunday, May 20, 2012

LONDONI WAONGEZA TIMU NYINGINE PREMIASHIP


Bao la Ricardo Vaz Te katika dakika za majeruhi liliapatia klabu ya West Ham ushindi na tikiti ya kurejea katika Ligi kuu ya Premiership baada ya msimu mmoja katika daraja la championship.
Carlton Cole
Carlton Cole
Klabu kutoka jijini London, West Ham ilipata bao la kwanza kupitia mshambuliaji wake Carlton Cole lakini likafutwa na Thomas Ince mtoto wa mchezaji wa zamani wa West Ham, Paul Ince mda mfupi baada ya kipindi cha pili kuanza.
Pande zote mbili zilikua na kosa kosa nyingi ingawa ni timu kutoka London iliyotumia fursa muhimu ambapo mshambuliaji Vaz Te aliyesajiliwa hivi katika dirisha la mwezi Januari kutoka klabu ya Barnsley, kujikuta peke yake na kupiga mpira kutoka umbali wa yadi 12 kuwainua mashabiki wa Hammers.
Bao hili pia lina maana kua West Ham imeweza kushinda mechi kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa Wembley katika kipindi cha miaka 31, na kurejea kwake baada ya kushuka daraja kwa kipindi cha mwaka mmoja wanafuata rekodi ya mwaka 1996 ya klabu ya Leicester.
Furaha ya West Ham hata hivyo, yaligeuka kua majonzi kwa Blackpool iliyoshuka daraja pamoja na West Ham msimu uliopita haikujaliwa kurejea katika Ligi kuu.
Msisimko ulijitokeza wakati mmoja ikionekana kama Blackpool inaweza kurudisha bao na kusababisha mda wa ziada wa kuamua mshindi lakini kujeruhiwa kwa mshambuliaji Gary Taylor Fletcher kulipunguza matumaini na kuiongezea West Ham matumaini.
Big Sam
Big Sam

No comments:

Post a Comment