Waandishi Wetu
SIMANZI,
huzuni na vilio viliwatawala wanamichezo nchini baada ya kupata taarifa
za kifo cha kiungo wa kimataifa wa Rwanda na Simba, Patrick Mutesa
Mafisango (32) aliyefariki dunia jana alfajiri kwa ajali ya
gari.Mafisango anatarajiwa kuagwa leo kwenye Uwanja TCC Sigara
Chang'ombe jijini Dar es Salaam kabla ya kesho kusafirishwa kuelekea
nyumbani kwao DR Congo kwa mazishi .
Msemaji wa Simba, Ezekiel Kamwaga alisema taratibu za kuuaga mwili wa marehemu zitaanza saa nne asubuhi mpaka saa 10 jioni.
Mafisango
alipata mauti hayo eneo la Veta Chang'ombe usiku wa kumkia jana saa
8.45 alipokuwa akiendesha gari akitokea Maisha Club akiwa na wenzake
wanne na alipofika maeneo ya Veta wakati akijaribu kumkwepa mwendesha
baiskeli ya miguu mitatu 'Guta' gari lilimshinda na kugonga mti
uliosababisha gari yake kuingia mtaroni na mauti kumkuta hapo hapo.
No comments:
Post a Comment