Wednesday, May 16, 2012

BIBI. MWAJUMA NYAMKA ameipongeza ...............

Ben Komba/Pwani-Tanzania/Wednesday, 16 May, 2012/19:27:06

Katibu wa chama cha mapinduzi wilaya ya Kibaha, BIBI. MWAJUMA NYAMKA ameipongeza halmashauri kuu ya chama chake kuhusiana na suala zima la kuamua kusimamia kidete suala la uwajibikaji kwa lengo la kuharakisha maendeleo.

Akizungumza na mwandishi wa habari ofisini kwakeBIBI. NYAMKA amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi kimeamua kuchukua hatua za makusudi kusisitiza uwajibikaji na kuhakikisha kuanzia sasa mtu ambaye atapewa nafasi yoyote ya uongozi, chama kitabidi kujiridhisha na uaminifu wake ili kupata vioingozi bora na sio bora viongozi.

Ameongeza kwa upande wao Chama Cha Mapinduzi wilayani Kibaha kilishaanza kuchukua hatua hizo kutokana na kutambua kuwa kiongozi wa CCM ni sawa kuwa kiongozi wa serikali na hivyo ni wajibu wao kupanga safu upya katika kuhakikisha Chama chao kinajiimarisha ili kuwatumikia wananchi kikamilifu.

BIBI. NYAMKA amewahakikishia wananchi na wanachama wa chama cha mapinduzi kwamba kupitia chaguzi za ndani ya chama na jumuiya zake zinazoendelea kwa sasa nchi nzima, kitu ambacho kitazingatiwa ni kupata viongozi bora ambao hawatajali maslahi binafsi na mabao wajua wajibu wao kwa chama na nchi bila kusubiri kusukumwa, ikiwa pamoja na kupambana na rushwa katika uchaguzi huo ili kujenga imani kwa wananchi na wanachama wa chama hicho.

No comments:

Post a Comment