Monday, January 23, 2012

Vifo zaidi mjini Kano, Nigeria


Hasara baada ya shuambulizi la Boko Harama
Idadi ya vifo viliyotokana na shambulio la bomu siku ya ijumaa lililofanywa na kundi la kiislamu huko Nigeria inaongezeka , hayo ni kwa mujibu wa madaktari.
Maafisa wa hospitali wanasema watu mia moja hamsini wamethibitishwa kuuawa lakini miili ya watu hao bado inaendelea kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti.
Boko Haram , wanaodai kuundwa kwa jimbo la kislamu wamesema sababu yao ya kufanya shambulio hilo ni kuwa vyombo vya kiusalama vimekataa kuwaachia huru wanachama wao waliokamatwa.
Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria alitembelea eneo hilo la Kano kuwafariji waathiriwa.
Amesema hali ya kiusalama Nigeria wakati huu ni nyeti zaidi ikilinganishwa na ilivyokuwa wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1967-1970.
Hata hivyo ameapa kupambana na walioishambulia mji wa Kano .
Katika muda wa mwaka mmoja sasa Boko Haram wamefanya mashambulizi kadhaa , katika makanisa, majengo ya serikali na hata vituo vya polisi na kusababisha vifo vya mamia ya watu.
Katika ziara ya Kanu Umma uliojitokeza kumuona rais Goodluck ulidhibitiwa vikali na walinzi wake na pia wanajeshi. Katika ziara hiyo fupi ,msafara wa kiongozi huyo uliokuwa na ulinzi mkali, pia ulitembelea hospitali wanakotibiwa majeruhi, na kuzuru maeneo yalioharibiwa kwa mabomu siku ya ijumaa .
Rais Jonathan amenukuliwa kusema 'mashambulio haya ya kujitoa muhanga ni mapya sana kwetu'.
Inakadiriwa idadi ya waliokufa inaweza kufika 250. Polisi mmoja katika eneo hilo amesema washabulizi Boko Haram wapatao 50 walimudu kuwatorosha wafungwa kutoka kituo cha polisi.

No comments:

Post a Comment