Wednesday, January 4, 2012

SHAMBULIO LA BOMU HUKO RWANDA


Rais wa Rwanda Paul Kagame
Rais wa Rwanda Paul Kagame
Takriban watu 18 wamejeruhiwa kufuatia shambulio la gurunedi lililotokea mjini Kigali, Jumanne usiku .
Maafisa wa polisi wamesema hakuna mtu aliyeuawa kufuatia shambulio hilo kufikia sasa.
Bado haijafahamika ni nani waliohusika na shambulio hilo, lakini polisi wanasema upelelezi umeanzishwa.
Mwanamke mmoja alielezea BBC alichoshuhudia, ''Nilikuwa nakwenda kuchukua simu yangu nikasikia mlipuko mkubwa, tukaanguka hapa na pale, wengi walinilalia wale waliokuwa nyuma yangu ndio waliojeruhiwa vibaya sana'' amesema .
Mwanamke huyo anasema kulikuwa watu wengi katika eneo la tukio na wengi wamejeruhiwa vibaya na kwamba wengine walipekelekwa hospitalini wakiwa hali mahututi.
Shambulio hilo limetokea katika soko moja katika eneo la Gasambo, mjini Kigali, lenye msongamano mkubwa wa watu.
Shambulio hilo limetokea mwaka mmoja baada ya mfululizo wa mashambulio ya magurunedi yaliyokumba mji wa Kigali, ambapo washukiwa 30 walifikishwa mahakamani.

No comments:

Post a Comment