Tuesday, January 10, 2012

QPR YAMNASA HUGHES

Mark Hughes 'amekubali kimsingi' kuwa meneja mpya wa QPR, 
Mark Hughes alipewa nafasi kubwa ya kuchukua nafasi ya Neil warnock, na baada ya mazungumzo siku ya Jumanne, alisema: "Tunatakiwa kujadili masuala kadhaa, lakini mazungumzo yalikwekda vizuri."
Mwenyekiti wa QPR Tony Fernandes aliandika kwenye ukurasa wake wa Tweeter siku ya Jumanne: "Ndio nina hakika tutakuwa tukitangaza meneja mpya wa QPR leo."
QPR iko katika nafasi ya 17n katika ligi kuu ya England na wamecheza mechi nane bila ushindi.
Mkurugenzi mkuu wa QPR Philip Beard alisema siku ya Jumanne: "Nadhani tutakamilisha mambo yote leo.
"Tunataka kuelewa kutoka kwa Mark jinsi anavyohisi kujihusisha na wamiliki wa QPR.
"Tuna imani Hughes atakuwa amefikiria usiku wa leo."
Hughes, akizungumza nje ya uwanja wa Loftus Road baada ya mazungumzo wa Jumatatu alisema: "Kuna mengi zaidi ya kujadili na tutasubiri hadi asubuhi.
"Bado tunajadili mawazo ambayo klabu inayo. Nimefurahishwa na jinsi hali inavyokwenda lakini hakuna kilichothibitishwa.
QPR ilianza kwa kasi mwanzo wa msimu, baada ya kurejea katika ligi kuu ikiwa chini ya Warnock, na kushika nafasi ya tisa, mwezi Novemba.
Lakini bila ushindi wowote tangu wakati huo, QPR imeporomoka hadi nafasi ya 17.

No comments:

Post a Comment