Tuesday, January 10, 2012

MTOTO WA GADDAFI

Siku ya mwisho iliyotolewa kwa Libya na Mahakama ya Kimataifa ya ICC kuhusu taarifa na afya ya Saif al-Islam Gaddafi imekaribia kumalizika.
Mtoto wa kiongozi wa zamani wa Libya alikamatwa kusini mwa Libya mwezi Novemba.
Mahakama ya ICC, yenye makao yake makuu The Hague, inamtaka kwa uhalifu dhidi ya ubinaadam, lakini viongozi wapya wa Libya wanasema wanataka kesi yake isikilizwe Libya.
Mahakama ya ICC huenda ikafikisha suala hilo katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa iwapo Libya haitajibu madai ya taarifa hizo mwisho wa siku ya Jumanne.
ICC imekubali kuwa Saif al-Islam ashtakiwe nchini Libya, lakini inataka kuhakikishiwa kwamba mfumo wa kisheria wa Libya utaendesha kesi kwa njia ya haki.
Katika ziara yake nchini Libya mwezi Novemba, mwendesha mashtaka mkuu wa ICC, Luis Moreno-Ocampo alisema: "Msimamo wa ICC ni kuwa lazima kuwe na mchakato wa kisheria ambao hautakuwa unamkinga mshukiwa.. Na ninaheshimu uamuzi wa kesi kusikilizwa nchini Libya... na si kama tunaogombea kesi hii."
Saif al-Islam, mtoto maarufu zaidi wa Kanali Gaddafi, anashikiliwa katika mji wa magharibi wa Zintan. Alikamatwa wakati akijaribu kutoroka nchi hiyo.
Saif al-Islam Gaddafi al;iwaambia wawakilishi wa shirika la kutetea haki za binaadam la Huma Rights Watch mwezi uliopita kuwa alikuwa akitunzwa vyema, lakini hakuwa amekutana na wakili yeyote au kuelezwa mashtaka dhidi yake.
Fred Abrahams wa Huma Rights Watch ameiambia BBC kuwa kwa jinsi alivyomuelewa katika mkutano wao, Saif al-Islam "haelewi kikamilifu kwamba yeye sio mtu mwenye nguvu tena nchini humo".
Mwandishi wa BBC Gabriel Gatehouse, ambaye yuko mjini Tripoli, anasema kesi ya mtoto wa kiongozi huyo wa zamani anashtakiwa kwa uhalifu wa kivita jambo ambalo halitakuwa kipaumbele kwa wanaharakati wa haki za binaadam.

No comments:

Post a Comment