Umoja wa Mataifa umeonya kuwa
shughuli za misaada ya dharura ya kibinadamu zitaathiriwa vibaya katika
nchi ya sudan kusini kutokana na mapigano ya kikabila yaliyofanyika
katika wiki za hivi karibuni nchini humo.
Sasa inakadiriwa kuwa zaidi ya watu laki moja na
elfu ishirini wanahitaji msaada, idadi hiyo ikiwa ni zaidi ya mara dufu
ya wale waliouhitaji awali.Mfululizo wa mashambulio ya kuvizia ya wafugaji katika jimbo la Jonglei ulisababisha mapigano baina ya makabila ya Lou Nouer and Murle mwezi uliopita.
Watu wengi waliuawa na maelfu ya watu wameyakimbia makazi yao kutokana na mapigano hayo.
Maafisa wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan kusini wamekanusha hutuma kuwa walizorota kushughulia suala hilo ipasavyo mapema.
Migogoro ya kikabila ya mara kwa mara imekuwa ikitishia hali ya usalama wa taifa hilo jipya zaidi barani Afrika
No comments:
Post a Comment