Sunday, January 29, 2012

BOKO HARAMU WAUWAWA

Jeshi la Nigeria linasema limewapiga risasi na kuwauwa wafuasi 11 wa kikundi cha wapiganaji wa Kiislamu, Boko Haram, kaskazini-mashariki mwa nchi.
Watu waliouliwa na Boko Haram
Msemaji wa jeshi alieleza kwamba wapiganaji hao waliuwawa wakati wa mapambano katika mji wa Maiduguri, ambako kundi hilo lilianzishwa mwongo uliopita.
Juma lilopita watu kama 185 waliuwawa katika mji mwengine wa kaskazini, Kano, kwenye mashambulio kadha ya mabomu.
Boko Haram ilisema ilifanya mashambulio hayo, na imeonya kuwa itaendelea na ugaidi hadi mfumo wa sharia unafuatwa Nigeria nzima.

No comments:

Post a Comment