Tuesday, December 27, 2011

VIFO 1500 HUKO FILIPINS "PHILIPPINES"

IDADI YA WATUWALIOKUTWA NA JANGA LA MAFURIKO KUSINI MWA UFILIPINO IMEFIKIA 1500 NA WENGINE WENGI WAKIWA HAWAJULIKANI WALIPO NA WENGINE WAKIPOTEZA MALI NA MAKAZI YAO. MAOFISA WA HUKO WANASEMA MIILI ZAIDI IMEKUTWA KATIKA KISIWA CHA MINDANAO. MAFURIKO HAYO YAMETOKEA BAADA YA KIMBUNGA "WASHI" KUIKUMBA NCHI HIYO KWA SIKU KADHAA KUANZIA DESEMBA 16 HADI 18.INASADIKIWA KUA IDADI KUBWA YA WALIOKUFA, WALIKUTWA NA KIMBUNGA HICHO KIJULIKANACHO KAMA "WASHI" WAKIWA WAMELALA. KIMBUNGA HICHO KILIKUA NA NGUVU KUBWA MNO AMBAPO KILISABABISHA KINGO ZA MITO KUVUNJIKA NA KUTOKEA KWA MAPOROMOKO YA UDONGO NA INADHANIWA KUWA KIJIJI KIMOJA KIMETOKOMEA CHOTE MAJINI.

No comments:

Post a Comment