Thursday, December 1, 2011

NAFASI YA OCAMPO

Jaji mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman ni mmoja kati ya watu wanne muhimu wanaoweza kushika nafasi ya Mwendesha Mashtaka katika Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa iliyoko The Hague, nchini Uholanzi.

Nafasi hiyo ambayo kwa sasa inashikiliwa na Luis Moreno-Ocampo itakuwa wazi hapo mwakani baada ya Bw Ocampo kumaliza kipindi chake cha utumishi wa miaka tisa mwakani.
Taarifa zinazohusiana
UN,
Tanzania

Kwa mujibu wa shirika la habari la AF, wagombea wengine ni pamoja na Naibu Mwendesha Mashtaka wa sasa Fatou Bensouda wa Gambia, ambaye wengi wanamwona kuwa analeta ushindani mkali.

Anaungwa mkono na Umoja wa Afrika ambao mara nyingi umemkosoa Moreno-Ocampo kwa kufungua uchunguzi wa mataifa ya Afrika pekee.

Jaji Othman ameshika nafasi muhimu mbalimbali za uandamizi katika mfumo wa sheria nchini Tanzania na alikuwa mwendesha mashtaka mkuu katika mahakama maalum ya mauaji ya Rwanda na pia mwendesha mashtaka katika Utawala wa Mpito wa Umoja wa Mataifa katika Timor Mashariki.

LAKINI KWA MUJIBU WA WACHUNGUZI WA MAMBO WANASEMA RAIA WA GAMBIA Fatou Bensouda anatarajiwa kutajwa kuwa mwendesha mashtaka mkuu mpya wa mahakama ya kimataifa ya ICC......STAY TUNE KWA HABARI ZAID.

No comments:

Post a Comment